Basi la Simba Mtoto Lapata Ajali Chamwino, 5 Wajeruhiwa!

Basi la Simba Mtoto Lapata Ajali Chamwino, 5 Wajeruhiwa!

Basi la Simba Mtoto Lapata Ajali Chamwino, 5 Wajeruhiwa! 

Basi la abiria kampuni mali ya Kampuni ya Simba Mtoto linalofanya safari zake kati ya Dodoma na Tanga limepata ajali mbaya majira ya sa 12 alfajiri katika Kijiji cha Chinangali, Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kujeruhi watu watano baada ya kugongana na lori la mizigo.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina la Michael ambaye pia ni mwanachama wa wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Dodoma aliyekuwa akisafirisha mdogo wake kutoka Dodoma kwenda shuleni Tanga, akizungumza na Global Publishers, amesema;

Basi la Simba Mtoto Lapata Ajali Chamwino, 5 Wajeruhiwa!

“Taarifa nilipata mapema kwa kuwa mimi pia ni nilikua nikimsafirisha mdogo wangu anayerejea shule kuendelea na masomo yake mkoani Tanga, yeye alipandia njiani maeneo ya Njiapanda ya Chamwino ambapo kuna kituo cha kupakia abiria.

 

“Baada ya kupewa taarifa ya ajali nilifika eneo la tukio haraka na kuwapigia simu wanachama wenzangu waliopo katika kata yangu ili kuweza kutoa msaada wa huduma ya kwanza kwa majeruhi.

Basi la Simba Mtoto Lapata Ajali Chamwino, 5 Wajeruhiwa!

“Tulikuta majeruhi watano lakini hakukuwa na kifo, tuliwapa taarifa uwongozi wa Mkoa ambao walifika haraka wakiongozwa na Mratibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Dodoma, Michael Mshingo. Walifika eneo la tukio wakiambatana Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Haraka tuliwanasua majeruhi wote na kuwakimbiza katika hospitali.

 

“Ninamshukuru Mungu, mdogo wangu amepata majeraha madogo madogo maeneo ya kichwani, kuchubuka shavuni, mikononi na mgongoni lakini kwa sasa amepelekwa hospitali kwa matibabu Zaidi,” amesema shuhuda huyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post