Bangala Asajiliwa na Azam Fc


Bangala Asajiliwa na Azam Fc

Yanga SC wametangaza kuwa wamefikia makubaliano na Azam FC juu ya uhamisho wa Mchezaji Yanick Litombo Bangala Raia wa Congo DR kutoka Yanga kwenda Azam FC.

Bangala alijiunga na Yanga mwaka 2021 na amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga kilichosaidia kutwaa mataji mbalimbali ya Ligi Kuu mara 2, ASFC mara 2 na kucheza fainali ya CAF na na kuibuka na tuzo ya Mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022.


Bangala ameuzwa kwenda Azam FC kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri ila tetesi zikisema ni Tsh milioni 100, hivyo kuwasili kwake Azam FC kuna muweka shakani Mnigeria Issah Ndala ambaye huenda akakatwa ili kufanya idadi ya Wachezaji wa kigeni kusalia 12.

Post a Comment

Previous Post Next Post