Yanga yasajiri mshambuliaji kutoka ghana - Hafiz Konkoni

Yanga yasajiri mshambuliaji kutoka ghana - Hafiz Konkoni

 Yanga SC wametangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana Hafiz Konkoni (23) kutokea Club ya Bechem United ya Ghana.

Hafiz katika msimu uliopita wa Ligi Kuu nchini Ghana alibuka nafasi ya pili kwa wanaowania Tuzo ya Mfungaji bora kwa kufunga magoli 15 na assist 3 katika michezo 26 aliyocheza.

Bado Yanga hawajaweka wazi wamempa Mkataba wa muda gani Mshambuliaji huyo ambaye inatajwa kuwa ndio mbadala wa Fiston Kalala Mayele aliyeondoka katika Timu hiyo na kuhusishwa kwenda Pyramid FC ya Misri.

Post a Comment

Previous Post Next Post